UMEKUTANA na msichana wa sampuli uliyokuwa ukiiota tangu utoto wako na amekukubalia kuwa atakuwa mpenzi wako, au pengine tayari mmekubaliana kufunga ndoa. Hiyo ni hatua kubwa ambayo unapaswa kujipongeza kwa kuifikia, kwani si wote wanaoweza kufanikiwa kuwapata wanawake walio katika viwango walivyovitaka wao. Hata hivyo, unakabiliwa na mtihani mwingine. Ni msichana unayempenda sana na umepanga kuwa umpe mapenzi ya hali ya juu, katika maisha ya kawaida na kitandani pia. Pengine katika mazungumzo yako pia uliashiria kuwa u mjuzi katika suala zima la mapenzi. Vilevile, yamkini akilini mwako umejijengea mawazo kuwa njia ya kwanza kabisa ya kumwonesha msichana wako kuwa kwako amefika, ni kumpagawisha kimapenzi unapokutana naye kimwili kwa mara ya kwanza. Lakini bahati mbaya, kuna upande mwingine wa shilingi katika suala hili. Wakati ukipanga hivyo, unaweza kujikuta kuwa umeingia katika shinikizo kutokana na mshawasha ulio nao, kiasi kwamba ukaanza kuwa na wasiwasi kama kweli utamfurahisha mpenzi wako siku ya kwanza. Ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi ya siku ya kwanza ni ya kihistoria hasa kwa mwanamke na kuna makubaliano miongoni mwa wataalamu wa saikolojia ya mapenzi kuwa mwanamke anapofurahishwa siku ya kwanza hujenga mapenzi makubwa kwa mwanaume aliyempa furaha hiyo, hususan kama ni mara yake kushiriki tendo la ngono. Sasa je, uko tayari kuona mwanamke uliyemhangaikia kwa siku nyingi mpaka akakukubalia anakata tamaa na kukupuuza siku ya kwanza tu ya kukutana nawe? Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayetamani kuingia katika hali hii. Ni wazi kuwa ungependa kujijengea jina na mapenzi makubwa kwa mwanamke wako huyu maridadi. Ili kukusaidia wewe ambaye umempata mpenzi na una wasiwasi kuwa pengine unaweza kuvuruga kila kitu katika siku ya kwanza, hapa yatabainishwa mambo kadhaa ambayo ukiyazingatia hutapaswa kuwa na shaka. Lakini hatua ya kwanza kabisa ni kujisikia huru. Suala la kukutana kwa mara ya kwanza na mpenzi huonekana kuwatisha wengi kuliko inavyopaswa. Katika kukabiliana nalo, jisikie huru kwanza na nafsi yako, kisha na mtu uliye naye, halafu mambo mengine yatafuata. USIHOFIE MAUMBILE YAKO Baadhi ya wanaume huwa na wasiwasi na maumbile yao. Katika zama hizi habari kuhusiana na masuala ya maumbile zimetapakaa kila mahala na mtu anaweza kujilinganisha na kujiona kama yeye hafai, mathalani ni mfupi. Kwa sababu hiyo, mwanaume atakuwa na wasiwasi kuwa mpenzi wake 'hatamtambua' vizuri, hususan katika siku hiyo ya kwanza na pengine huo utakuwa mwanzo wa kumdharau kisha kumwacha. Ni kweli kuwa kwa baadhi ya wanawake urefu unaweza kuwa na maana. Naam, ni suala la kawaida kuwasikia baadhi ya wanawake wawazi wakisema kuwa wao hawawapendi wanaume wafupi (kwa maana zote za ufupi). Lakini urefu hauwezi kuwa mbadala wa mapenzi ya kweli. Pia, baadhi ya wanawake hawaamini zaidi katika urefu, bali zaidi ufundi na ustadi wa mwanamume katika wajibu wake. Huo unaweza kuwa ukweli kwa kiasi kikubwa, kwani kama unafahamu jinsi ya kumfurahisha mwanamke kwa njia nyingine basi kumwingilia inapaswa kuwa hatua ya mwisho. Katika kukabiliana na hofu kuhusiana na maumbile yako, hakikisha kuwa unatoa nafasi katika mchezo wa awali kabla ya tendo lenyewe, ili kumwonesha jinsi ulivyo mtaalamu, kwa kutumia vidole vyako, ulimi wako na kila kinachowezekana (ikizingatiwa kuwa tayari mmeshapima na kuthibitika kutokuwa na magonjwa ya ngono, au mkizingatia kinga). Gusa sehemu za mwili wake ambazo mara nyingi watu huzipuuza wanapokuwa katika mapenzi na kukimbilia sehemu inayopaswa kushughulikiwa ikiwa ya mwisho na unapoamua kuwa sasa unaingia ndani, ingia huku ukijiamini, ukiwa huna wasiwasi na maumbile yako. Hapo mambo yatakuwa rahisi maana kazi kubwa umeshaifanya. Hata kama ni kweli kuwa maumbile yako ni madogo, chini ya wastani unaoelezwa kisayansi, bado unayo nafasi ya kuifanikisha kazi vizuri na kumfikisha kileleni mpenzi wako, tena pengine ikiwa mara ya kwanza kwake kufika kileleni. Kwa ujumla, usikubali urijali wako uamuliwe na ukubwa au udogo wa maumbile yako. ONDOA SHINIKIZO Kabla ya kukutana kimapenzi kwa mara ya kwanza, ni kawaida kwa kila mmoja kuwa na shinikizo, akifikiria jinsi mwenzake atakavyomchukulia. Kwa upande wa mwanamume, kulifikiria sana tendo la ngono husababisha shinikizo. Hali hii husababisha damu nyingi kujikita katika ubongo hivyo kupunguza uwezo na nguvu za kiume, kwani nguvu zimeelekezwa katika ubongo kwa ajili ya kuwaza na kufanya tafakuri kuhusiana na kile mtu anachokwenda kukivumbua. Hili ni suala la kisayansi, kwani kitu ambacho huufanya mwili wa mwanamume (hususan uume) kusisimka katika mazingira ya mapenzi, ni kukusanyika kwa damu kutoka katika sehemu mbalimbali za mwili na kujaa katika mishipa yake, lakini sasa nguvu zimeelekezwa kwenye ubongo na damu imekimbilia huko. Katika suala la ngono, jambo ambalo unapaswa kulifikiria zaidi si kuuona utupu wa mwanamke, wala kutafakari jinsi atakavyokuwa anahangaika, bali jinsi utakavyofurahia tendo lile. Sahau matatizo yako, mawazo yako yote elekeza kwenye furaha iliyo mbele yako. Kama vile ambavyo mwanamke hupaswa kujituliza kiakili ili aweze kuwa katika hali njema ya kushiriki tendo la ngono, mwanaume pia hupaswa kuweka sawa mawazo yake, akijiandalia furaha iliyo mbele yake. Kama unahisi kuushinikiza ubongo wako kwa mawazo, fumba macho yako na kuruhusu milango mingine ya fahamu kufanya kazi, ukiwa tayari chumbani na mpenzi wako. Zaidi ya hapo, zungumza na mpenzi wako kuhusiana na mambo ambayo humletea hisia za kimapenzi. Kuwa na subira unapoiendea furaha yako na unapokuwa tayari kuingia katika upeo wa furaha yako, elekeza mawazo yako yote kwake na si kwenye nafsi yako, usije ukabaini mapungufu yanayoweza kukukwaza. Na kama pengine ulikuwa na wasiwasi kuhusiana na magonjwa ya kuambukiza au mimba, chukua uamuzi haraka kabla ya kukutana na mpenzi wako. Mathalani, ni vema kama mtakuwa mmepima, kama hamkupima basi tumia kondomu ili kuwa na amani. HOFU YA KUMALIZA MAPEMA Kutokana na mshawasha uliokuwa nao kwa siku nyingi, kuna hatari kubwa ya kufikia kilele katika sekunde tano tu na kumwacha mwenzako akihangaika. Yawezekana hilo ndilo tatizo linalokusumbua – una wasiwasi kuwa utafika kileleni kabla mwenzako hajakufaidi. Wasiwasi huo unaonesha kuwa unamjali mwenzako. Ili kuepukana na aibu ya kufika kileleni katika muda wa sekunde chache, epuka msisimko wa moja kwa moja. Unapohisi kuwa unataka kufika kileleni mapema, punguza kasi na kuelekeza mawazo kwingine. Pia waweza kufanya matendo mbadala kwa kutumia vidole na ulimi, au kubadilisha mkao mara kwa mara. HOFU YA KUTOMFIKISHA KILELENI Katika zama hizi, vijana wengi wamekuwa wakijitahidi kuwafikisha wapenzi wao katika kilele cha furaha zao, kutoka na tafiti zinazoonesha kuwa baadhi ya wanawake huishi maisha yao yote bila kufikishwa kileleni, kutokana na uzembe na ubabe wa wenzi wao. Lakini pamoja na jitihada zote unazoweza kuzifanya ili kuhakikisha kuwa jambo hili linafanikiwa, ukweli ni kwamba mwanamke mwenyewe pia anawajibika kutoa mchango wake, kwani raha atakayopata kwa kufika kileleni itakuwa yake. Kama mwanamke hajawahi kufika kileleni maishani mwake, basi pengine hupaswi kuwa na shinikizo lolote katika suala hili, lakini kama utaazimia kuhakikisha anafika kileleni, basi anza kushughulika kwanza na akili yake, kabla hujaingia kwenye maeneo mengine ya mwili wake. Zungumza naye kuhusiana na mambo mbalimbali ya kusisimua na unapomgusa baadaye, mguse taratibu na kwa hesabu, ili kumfanya atafakari yale uliyokuwa unamwambia kabla hujaanza kumgusa. Ni muhimu sana kumwanzia mwanamke kwa mwendo mdogo, ukawa unaongeza taratibu kadiri anavyokolea. Usiogope kutumia vidole vyako, kinywa chako na ulimi wako. Vipo viungo mbalimbali katika mwili wa mwanamke ambavyo vitakusaidia katika kazi yako ya kumpeleka kileleni, lakini bahati njema ni kwamba yeye pia anataka kufika kileleni. USIOGOPE, UNAWEZA Usipokuwa na wasiwasi wa kushindwa, mapenzi ya kukutana kimwili ni kitu rahisi, kwani ni cha asili. Wewe ni mwanaume na unapaswa kujiamini katika kila jambo unalolifanya, ikiwa ni pamoja na suala la ngono. Kama utajiaminisha kuwa unaweza kufanya ngono kwa umahiri na kumfurahisha mwanamke, ukweli ni kwamba utaweza.
FARAJI
Friday, 5 August 2016
Tuesday, 26 July 2016
HAKUNA CHUO KILICHOFUNGIWA- TCU
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewatoa hofu wanafunzi waliohitimu katika vyuo vilivyozuiwa hivi karibuni kufanya udahili, huku ikikanusha taarifa za kuzifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi.
Hivi karibuni TCU ilitangaza kusimamisha kufanya udahili vyuo vitano baadhi vikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis cha Ifakara Morogoro, Chuo cha Mtakatifu Joseph cha Dar es Salaam na Chuo cha IMTU cha Dar es Salaam vyote kwa kozi ya udaktari.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Eliuther Mwageni alisema kufungiwa kwa vyuo hivyo ni kwa muda mpaka vitakapokabidhi vigezo vinavyotakiwa.
Mwageni alisema…….>>>”Kuna vigezo vinavyotakiwa kufikiwa ili chuo kiweze kusajiliwa na hivi vyuo hatujavifungia ila tumevisimamisha kwa muda mpaka vikidhi vigezo vyetu.
Kuhusu taarifa za vyuo 22 kusimamishwa kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali zilizozagaa kwenye mitandao juzi na jana, Mwageni alisema……>>> ‘taarifa hizo ni za uzushi, zina lengo baya hivyo hazina ukweli wowote‘. KUTOKA MILLARD AYO
Source: Gazeti la Jambo Leo